Betrand Bisimwa, kiongozi wa waasi wa zamani wa
kundi la M 23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesema ripoti ya
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch
kuwa wapiganaji wake walitumiwa na serikali ya Kinshasa, kuwakabili
waandamanaji mwaka uliopita ni uongo.
Bw
Bisimwa amesema wapiganaji walionekana kusajiliwa na serikali ya
Kinshasa ni wale waliokuwa wameondolewa katika kundi hilo muda mrefu.
Serikali
ya DRC nayo pia imekanusha ripoti hii ya Human Rughts Watch, huku
Shirika hilo likisema uchaguzi wao umebaini ukweli huo baada ya
kuzungumza na waasi hao wa zamani pamoja na familia zao.
Mapema
wiki hii shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch
lilimtuhumu rais Joseph Kabila kuwasajili wapiganaji wa zamani wa kundi
la M23 kwa lengo la kuwakandamiza waandamanaji waliokuwa wakipinga
utawala wake Desemba 19 na 20 mwaka 2016 jijini Kinshasa.
Kwa mujibu wa shirika hilo, ukandamizaji ulisababisha vifo vya watu 60.
Serikali
ya DR Congo kupitia waziri wake wa haki za binadamu Marie Ange
Mushobeka, alisema ameshangazwa na ripoti hiyo na kwamba shirika hilo
halina ushahidi wowote kuhusu tuhuma hizo.
Hata hivyo Human Right
Watch inasema ilikusanya ushahidi kupitia watu mbalimbali wakiwemo
wapiganaji hao waliotoa ushuhuda kama anavyoeleza hapa Ida Soyere
mkurugenzi wa Human Right Watch katika ukanda wa Afrika ya kati.
No comments