Rais
wa Marekani Dnald trump anaendelea kukabiliwa na vitisho vya kuvunjika
kwa uhusiano wa kidiplomasia wa nchi hiyo na jumuiya ya nchi za Kiarabu
kufuatia nia yake ya kutaka kuhamishia ubalozi wa Marekani nchini Israel
katika mji wa Jerusalem kutoka mji wa Tel Aviv.
Kama
kweli atachukua uamuzi huo kama alivyomtaarifu kiongozi wa Mamlaka ya
Palestina Mahmoud Abbas na Mfalme wa Jordan au kuutambua mji huo
mtakatifu kama mji mkuu wa Israel, Donald Trump atakua amekwenda kinyume
na msimamo wa jumuiya ya kimataifa na viongozi wengi waliomtangulia
katika uongozi wa taifa la Marekani. Nchi za Kiarabu zimeendelea kutoa
onyo kufuatia hatua hiyo ya Marekani.
Ikulu ya White House
imethibitisha kuwa rais Donald Trump atazungumza leo Jumatano kuhusu
uwezekano wa kuhamishia ubalozi wa Marekani Jerusalem.
Kwa mujibu
wa msemaji wa ikulu ya white house Sarah Sanders amesema kuwa Trump
alizungumza na baadhi ya viongozi siku ya jumanne kuhusu mpango wake ya
kuhamishia ubalozi huo kutoka tel aviv kuupeka Jerusalem.
Viongozi
wa Palestina, Misri, Jordan na saudi arabia, wametoa onyo kwa rais
Trump kuwa kuhamishia ubalozi huo Jerusalem kutadhoofisha kabisa juhudi
za kuleta amani Mashariki ya Kati.
Siku ya Jumanne rais wa
Ufaransa Emmanuel Macron alisema kuwa ana wasiwasi kuwa rais huyo wa
Marekani anaweza kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Israel na Palestina wote wanadai kuwa mji huo ni mji wao mkuu.
Israeli
ilivamia eneo hilo la Mashariki mwa Palestina mwaka 1967 na kulifanya
kama eneo lake baadae. Uamuzi huu hautambuliwi kimataifa. Israeli inaona
mji huo kuwa mji wake mkuu.
Kwa upande wao, Wapalestina wanadai Jerusalem ya Mashariki kama mji wao mkuu wa baadae.
No comments