Hatimaye, Mwanahabari wa RFI Hausa, Ahmed Abba yuko huru baada ya kuwa jela kwa muda wa miezi 29.
Hatua hii inakuja baada ya Mahakama ya rufaa siku ya Alhamisi kumhukumu jela kwa kipindi cha miezi 24 , kwa kosa la kutotoa taarifa kuhusu makundi ya kigaidi, adhabu ambayo tayari alikuwa ameitumikia.
Abba
alikamatwa mwaka 2015, wakati akiwahoji wapiganaji wa Boko Haram ambao
ni magaidi wanaokabiliana na jeshi la Mataifa ya Afrika Magharibi,
likiongozwa na Nigeria.
Mwahabari huyo raia wa Cameroon,
alifunguliwa mashtaka ya ugaidi na kushirikiana na kundi hilo na
Mahakama ya Kijeshi na kupewa kifungo cha miaka 10 jela, adhabu ambayo
ilibadilishwa.
Kipindi hicho chote, Abba alikanusha madai hayo na kusema kuwa hakupewa nafasi ya kujitetea mbele ya Mahakama hiyo.
Baada ya kuwa huru, Abba amesema amefurahi sana na kuwashukuru wale wote waliomsaidia kutoa jela hasa uongozi wa RFI.
“Nimefurahi
sana. Nimefurahi sana kuwa huru kuelekea Sikukuu ya Krismasi. Nipo
hotelini na Mkuu wangu wa kazi, Yves Rocle, pamoja na Mawakili wangu na
mwenzangu Polycarpe Essomba,”
“Hii ni zawadi ya Krismasi. Familia
ya RFI ilifanya bidii kuhakikisha kuwa niko huru. Waliniunga
mkono.Mashirika yote ya kimataifa na ya Cameroon ya kutetea haki za
binadamu, waliniunga sana mkono. Asanteni sana,” alisema Abba.
Mkurugenzi wa RFI Cécile Mégie, amesema amefurahishwa sana na hatua ya kuachiwa huru kwa Abba.
No comments