Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa Mkutano na wadau wa Sekta ya
Uwindaji wa Kitalii ili kujadili mikakati ya kuimarisha sekta hiyo.
Hii ni pamoja na utekelezaji wa azma ya serikali ya kuanzisha
utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa
njia ya mnada. Mwenyekiti wa Mkutano huo atakuwa Waziri wa Maliasili na
Utalii Dk Hamisi A. Kigwangala, Wadau wote mnakaribishwa ili
kufanikisha lengo la Mkutano huo kwa faida ya sekta ya uwindaji wa
kitalii nchini na maliasili za nchi kwa ujumla.
Mkutano utafanyika tarehe 28 Desemba, 2017 saa nne asubuhi katika ukumbi wa LAPF, Dodoma.
No comments