Siku
tatu baada ya kuvunja baraza la mawaziri, rais mpya wa Zimbabwe
Emmerson Mnangagwa ametangaza baraza lake jipya la mawaziri ambalo
linaundwa na maafisa wa jeshi waliochangia kumshinikiza rais Robert
Mugabe kuachia ngazi
Rais Mnangagwa amemteua afisa mkuu wa jeshi kushikilia wizara muhimu katika serikali yake.
Afisa
wa ngazi ya juu katika jeshi aliyetangaza kwenye televisheni ya taifa
wiki nne zilizopita kwamba jeshi limechukua udhibiti, Jenerali Sibusiso
Moyo Waziri wa Mambo ya nje.
Nae Mkuu wa jeshi la angani Perence Shiri atashikilia wizara wa ardhi.
Mnangagwa ambaye aliapishwa siku ya Ijumaa Novemba 24, aliwahutubia wananchi wake, huku akiwataka kudumisha demokrasia.
Hata hivyo, Waziri wa zamani katika serikali ya Robert Mugabe Patrick Chinamas ameteuliwa kuwa Waziri wa fedha.
Serikali ya rais huyo mpya haijawashirikisha wansiasa wa upinzani kama ambavyo ilitarajiwa.
Bw
Mnangagwa alichukua hatamu ya uongozi wa Zimbabwe siku chache baada ya
mtangulizi wake Robert Gabriel Mugabe kuachia ngazi kwa shinikizo la
jeshi na chama chake kufuatia malumbano ndani ya chama chake kuhusu nani
atakaemrithi.
Bw Mugabe alimfuta kazi makamu wake Emmerson
Mnangagwa kwa kile mkewe Grace Mugabe alichokitaja kuwa alikua na njama
za kutaka kumpindua mumewe katika uongozi wa nchi, madai ambayo Bw
Mnangagwa alifutilia mbali na kusema ni uongo mtupu
Robert Mugabe
ambaye alijiuzulu kwenye uongozi wa nchi ya Zimbabwe akiwa na umri wa
miaka 93 atakua akilipwa mshahara wa dola 150,000 kila mwezi huku mkewe
Grace Mugabe akilipwa nusu ya hizo, yaani dola 75,000. Mugabe vile vile
amekubaliwa kupewa kiinua mgongo cha milioni 10,000,000, kwa mujibu wa
gazeti la Guardian.
No comments