DUNIA YAADHIMISHA SIKU YA KUPAMBANA NA VIRUSI VYA UKIMWI
Dunia inaadhimisha leo Ijumaa Desemba 1, siku ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Ugonjwa wa Sida umeendelea kuwaacha watoto wengi mayatima huku wengi wao wakiambukizwa ugonjwa huo na wazazi wao.
Afrika Kusini ina idadi kubwa ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi duniani
Watu milioni 17.1 wameambukizwa virusi vya Ukimwi nchini humo, kulingana na ripoti ya mwaka 2016. Baada ya miaka ya kadhaa, Pretoria imepata mafanikio makubwa katika kuzuia makali ya ugonjwa huo, vipimo na matibabu ya wagonjwa wa Ukimwi.
Afrika Kusini ipo katika njia nzuri ya kufikia malengo yaliyowekwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalopiga vita Ukimwi (UNAIDS), ambalo linataka kuwa hadi mwaka 2020, 90% ya watu wanaoishi na VVU kujua hali yao, huku 90% ya watu walioathirika na VVU na waliopimwa, kupata matibabu na kwamba 90% ya wagonjwa wanaopata matibabu wawe wakipewa huduma ya kutosha.
Mamlaka ya Afrika Kusini inakadiria kuwa 86% ya watu walio na VVU nchini humo wanajua hali yao ya VVU kwa sasa. Baada ya vipimo, matibabu yamepewa kipaumbele kwa dhidi ya janga la Ukimwi nchini humo. Leo, watu milioni 4 wanapokea tiba ya kupambana na virusi vya Ukimwi nchini Afrika Kusini, kesi ya kipekee duniani.
Mabadiliko katika jamii dhidi Ukimwi
Juhudi zimenza kuzaa matunda: idadi ya vifo vinavyotokana na VVU imepungua kwa zaidi ya nusu tangu mwaka 2005. Miaka kumi na tano iliyopita, wagonjwa walikuwa wakipewa dawa tano kwa siku. Lakini tangu mwaka 2013, Wizara ya Afya ya Afrika Kusini ilipendekeza kuchukua kipimo cha kutosha, sawa na chembe ya dawa kwa siku.
Hata hivyo changamoto ni nyingi nchini Afrika Kusini katika mapambano dhidi ya Ukimwi, hasa kuendelea kuwapa matibabu wagonjwa, hasa katika maeneo ya vijijini.
Ufaransa, inakadiriwa kuwa na waathirika 6,000 wanaombukizwa kila mwaka.Katika hali ya kupunguza idadi hii, ambayo haijapanda au kupungua kwa miaka kumi, mbinu mpya zimeanza kuongezwa kwa kuongeza kondomu. Miongoni mwao mwa mbinu hizo ni pamoja na, PrEP, matibabu ya kuzuia makali ya virusi vya Ukimwi.
No comments