Ni miaka minne imepita tangu kifo cha Hayati Nelson Mandela ambaye alikuwakiongozi mashuhuri duniani ambaye alifariki Desemba 5, 2013.
Hata hivyo inadaiwa kuwa mazishi yake yalikumbwa na ufisadi mkubwa ambao unadaiwa kutekelezwa na viongozi wakuu nchini humo.
Mamlaka ya kupambana na rushwa nchini humo imechapisha ripoti yenye
kurasa 300, inayoonyesha jinsi gani urasibu mbaya na rushwa viligubika
matayarisho ya mazishi ya Nelson Mandela.
Kulingana na ripoti ya Mamlaka ya kupambana na rushwa nchini humo
takriban dola millioni 22 ilitumika vibaya wakati wa matayarisho ya
mazishi ya Mandela miaka minne iliyopita.
No comments