Majeshi ya Polisi ya Tanzania na Rwanda yameunganisha nguvu kupitia
Majeshi yao ya Polisi chini ya wakuu wake IGP Simon Sirro Tanzania na
RNP Emmanuel Gassana wa Rwanda ili kupambana na uhalifu, ujangili na
kuangalia namna ya kutatua matatizo yanayokumba nchi hizo.
Akizungumza na wanahabari leo akiwa Tanzania RNP Gassana amesema kuwa
lengo ni kushirikiana kutokana na changamoto ambazo zinatokea katika
nchi ikiwemo kuongeza nguvu, teknolojia, vifaa na kuongeza uzoefu wa
matumizi ya vifaa.
Kwa upande wa Tanzania, IGP Sirro amesema kuwa kwa ushirikiano huo ambao
unafanyika kwa kuangalia nini ambacho kinatakiwa kufanywa na maarifa
ambayo yatatumiwa ili Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake kwa
usahihi na kupunguza uhalifu na endepo mtu akijiingiza kwenye uhalifu
anaweza kupoteza familia yake na kuishia pabaya.
“Wenzetu Rwanda wako mbele katika matumizi ya teknolojia, hivyo kuna
baadhi ya mambo ambayo watatuelekeza na tutapata uzoefu katika kupambana
na wahalifu wa mitandaoni ambao wamekuwa wakiwasumbua raia. Sisi pia
tuna uzoefu wa mambo mengi ambayo wenzetu Rwanda watajifunza kutoka
kwetu,” amesema Sirro
No comments