Umoja wa Ulaya unatarajia kuwarudisha makwao
wahamiaji 15,000 waliokwama nchini Libya hadi mwezi Februari 2018, Mkuu
wa sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema leo alhamisi
mjini Brussels, nchini Ubelgiji.
Hili
ni lengo lililowekwa na kundi la wataalamu lililoundwa mwishoni mwa
mwezi Novemba katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa
Afrika mjini Abidjan, kwa kukabiliana na hasira iliyotokana na picha
zilizorushwa na vyombo vya habari kuhusu kuepo kwa masoko ya watumwa
nchini Libya.
Kundi hili linaundwa na Umoja wa Ulaya, Umoja wa
Afrika, IOM (Shirika la Kimataifa la linalohusika na masuala ya
wahamiaji) na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi
(UNHCR).
Kundi hili liliundwa kwa kukabiliana na hali mbaya ambayo
inawakabili wahamiaji waliokwama nchini Libya, kutoka Afrika na
Mashariki ya Kati, ambao wamekua wakijaribu kuingia Ulaya kwa kuvuka
bahari ya Mediterranean.
Siku ya Jumanne, shirika la kimataifa la
Haki za Binadamu la Amnesty International lilishutumu serikali za Ulaya
kuwa kuhusika katika katika njia moja ama nyingne kwa kuzuiliwa kwa
wahamiaji katikamazingira mabaya nchini Libya, ikizishtumu kuwasaidia
vikosi vya ulinzi wa baharini nchini Libya, ambavyo vinahusika katika
biashara haramu ya binadamu kwa mujibu wa shirika hilo.
No comments