Ripoti mpya ya shirika la kimataifa la haki za
Binadamu la Human Rights Watch inalaani uhalifu wa kijinsia, uliofanywa
na vikosi vya usalama, wakati wa uchaguzi wa Kenya mwaka mwaka huu.
Shirika
hili liliendesha uchunguzi wake katika vitongoji vya Nairobi na Kisumu
na Bungoma, magharibi mwa Kenya, katika ngome za upinzani.
"Watu
waliokua wakiendesha vitendo hivyo walikua wakivaa sare ya polisi.
Maneno haya, ambayo yamekua yakirejea katika ushuhuda wa waathirika,
yanathibitisha kuhusika kwa polisi katika vitendo viovu ikiwa ni pamoja
na ubakaji katika ngome za upinzani. Kati ya wanawake 65 waliohojiwa,
nusu yao wananyooshea kidole polisi.
Vitendo hivyo vilihusiana
moja kwa moja na uchaguzi, kulingana na ripoti hiyo. Mwathirika mmoja
amesema alibakwa mbele ya watoto zake, baada ya kukataa kusema kwamba
anamuunga mkono rais Uhuru Kenyatta. Mwingine ameelezea kwamba
alishambuliwa na watu ambao walikuwa wakisherehekea ushindi wa Uhuru
Kenyatta mbele ya maofisa wa polisi.
Human Right Watch inalaani vikwazo vingi vinavyozuia waathirika kupata huduma na kuwafungulia mashitaka wahusika.
Human
Rights Watch inadai kwamba wanawake na wasichana waliobakwa wakati wa
vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007, bado wanakabiliwa na matatizo ya
kimwili, kiafya na kisaikolojia.
Pia ripoti hiyo inasema serikali ya Kenya haijatoa usaidizi wa kimsingi kuwasaidia waathiriwa hao.
Kulingana na ripoti hiyo, zaidi ya visa 900 vya ubakaji viliripotiwa wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007.
Tangu
mkuanza kwa mgogoro nchini Kenya, mashirika yasiyo ya kiserikali
yamekua yakilaani ukatili unaofanywa na polisi. Watu zaidi ya 70
waliuawa katika makabiliano na polisi tangu uchaguzi wa kwanza wa urais
mnamo mwezi Agosti 2017. Tuhuma ambazo serikali imeendela kukanushaShare
No comments