VIJANA wanne na mtoto mmoja wamepandishwa kizimbani katika Mahakama
ya Wilaya ya Kinondoni kwa wizi wa kutumia mapanga na kuiba fedha na
vitu vyenye jumla ya thamani ya Sh milioni 3.35 Washitakiwa waliotenda
kosa hilo ni Dimas Denis (20), mkazi wa Kijitonyama, Juma Selemani (22)
anafanya kazi ya ulinzi mkazi wa Tandale Tanesco, Karimu Hamisi (23),
mkazi wa Ali Maua na mtoto wa miaka 17.
Wakisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Hanifa Mwingira, msoma
mashitaka Credo Rugaju alidai kwamba washitakiwa hao walitenda kosa hilo
Novemba 11 mwaka huu maeneo ya Ali Maua B, wilaya ya Kiondoni jijini
Dar es Salaam.
Alidai kwamba watuhumiwa hao waliiba, runinga flat Screen aina ya
Boss yenye thamani ya Sh 750,000, kompyuta mpakato aina ya Dell yenye
thamani ya Sh 800,000, simu aina ya Iphone Six Plus yenye thamani ya Sh
milioni 1.6 na fedha Sh 200,000 vikiwa ni mali ya Cresence Nguzo.
Rugaju alidai kwamba washitakiwa hao baada na wakati wakimuibia Nguzo
walimtishia kwa mapanga na kumuibia vitu hivyo. Washitakiwa wote
wamekana shitaka hilo, wamerudishwa rumande kwa kuwa makosa kama hayo
kisheria hayana dhamana. Washitakiwa hao wanatarajiwa kurudishwa tena
mahakamani hapo Desemba 27 mwaka huu, ili kutajwa kesi hiyo.
No comments