Waziri
Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi jana Jumamosi ametangaza ushindi dhidi ya
kundi la Islamic State nchini humo na kusema kuwa, sasa wanajeshi wa
Iraq wanadhibiti kikamilifu mpaka wa nchi hiyo na Syria.
Tangazo hili linakuja baada ya serikali ya Syria kusema kuwa imemaliza kazi ya kupambana na Islamic State nchini Syria.
Mamlaka
nchini humo zimetangaza mapumziko ya umma leo Jumapili kusherehekea
ushindi huo huku waziri mkuu Abad katika hotuba yake akiwa wizara ya
ulinzi amesema kuwa vita ya sasa nchini humo itakuwa kupambana na rushwa
.
Kundi la Islamic State limekuwa likipambana na vikosi vya
serikali ya Syria na Iraq tangu mwaka 2014 na lilifanikiwa kudhoibiti
maeneo mengi na makubwa nchini humo.
Wakati mamlaka zikitangaza
mapumziko ya umma leo Jumapili "kusherehekea ushindi", Abadi alisema
katika hotuba ya wizara ya utetezi kuwa vita vya Iraq ijayo itakuwa
kushinda janga la rushwa.
Naye kiomngozi wa kiroho wa taifa hilo
Ayatollah Ali Khamenei ,ametoa wito wa kuungana pamoja hatua
itakayosababisha kuundwa kwa vitengo vya silaha vya Hashed al-Shaabi.
No comments