Baada
ya kukutana na Rais wa Ufaransa mjini Paris siku ya Jumapili, Desemba
10, Waziri Mkuu wa Israel yuko ziarani Brussels kwa mkutano na Mawaziri
wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya.
Benjamin Netanyahu atakutana na mawaziri 28 wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wakati wa chakula cha asubuhi.
Waziri
Mkuu wa Israeli anaushtumu Umoja wa Ulayaku wa ni"wanafiki" juu ya
shutma dhidi ya uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kutambua
Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli.
"Ninaheshimu Umoja wa Ulaya
lakini siko tayari kukubali sera ya kuegemea upande fulani kutoka kwa
umoja huo," Bw Netanyahu amesema. "Wanashutumu tangazo la rais Trump,
lakini hawajashtumu kitendo cha kurusha roketi nchini Israeli,"
ameongeza.
Netanyahu anaweza kutofutilia mbali wazo la kutambua sehemu ya moja magharibi mwaJerusalem kama mji mkuu wa Israe.
Waziri
Mkuu wa Israel huenda akakubali ushawishi kutoka Umoja wa Ulaya lakini
kazi itakuwa ngumu, mwanahistoria Frédérique Schillo, amesema. "Anakuja
na ushindi mkubwa wa kidiplomasia, ambao ni kutambuliwa kwa Jerusalem
kama mji mkuu wa Israeli. Lakini anakuja Ulaya ambapo nchi wanachama wa
Umoja wa Ulaya wanapinga uamuzi huo wa Marekani juu ya Israel. Kwa
hivyo, atakua na kazi kubwa kushawishi washirika wake. Lakini bila
shaka, yuko atakua na kazi kubwa, kwani viongozi wa nchi hizi hawako
tayari kuunga mkono kutambua jerusalem kama mji mkuu wa Israel. "
Suala
jingine ambalo linaonekana kuwa litajadiliwa kati ya Netanyahu na
viongozi wa Ulaya katika mkutano wao mjini Brussels ni ukoloni wa
Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi. Waziri Mkuu wa Israel pia
atazungumia suala la kuwepo kwa Iran nchini Syria na Lebanon.
No comments