WAZIRI wa Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika amewaagiza
wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuwafukuza kazi mara moja waratibu wa
TASAF watakaobainika kusajili watu wasiostahili kuingizwa kwenye awamu
ya tatu ya Mpango wa Kuzinusuru kaya maskini kabla yeye hajafanya ziara
ya kutembelea katika maeneo husika.
Ametoa agizo hilo leo jijini Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja
iliyolenga kuelewa shughuli za TASAF pamoja na kutembela chuo cha
Utumishi wa Umma na kusema kuanzia sasa mkoa atakaoenda na kukuta tatizo
hilo linaendelea hatasita kuamchukulia hatua Mkurugenzi mtendaji kwa
kushindwa kuwajibisha wahusika.
Amesema kitendo kinachofanywa na waratibu hao katika baadhi ya
halmashauri cha kusajili watu wenye afya njema na akili timamu na
kuwaacha walengwa wakiwemo wazee hakiivumiliki katika utawala wa awamu
ya tano kwakuwa kinalenga kuiharibia serikali na kuvuruga malengo ya
utekelzaji wa mpango huo.
No comments