YANAYOKUPATA YANATOKA UNAPOKAA
YANAYOKUPATA YANATOKA UNAPO KAA
Kuna mambo mengi yanayoweza kumpata mtu, mambo haya yanaweza kuwa mazuri
yanayomfaa na kumpendeza au mabaya yasiyostahili kumkuta mwanadamu awaye yote
hapa duniani.
Mambo menge yanayompata mtu yanatoka mahali anapokaa au anapopendelea kuwa
mara nyingi.
Kuna watu wamepatwa na misukosuko na wengine kupoteza baadhi ya viungo vya sehemu za miili yao hata
maisha, kutokana na ugomvi uliotokea katika vijiwe wanavyo kaa , wengine
wamekutwa na hatia wameangukia kifungo kwa matukio mabaya yaliyo tokea, mahali
au kijiweni wanakokaa.
Vijana wengi wamepoteza mwelekeo wa maisha na hata kuzisababishia familia
zao matatizo makubwa kwa kupotoshwa na makundi wanayoyapendelea kukaa.
Wengine wameingia katika ugomvi mbaya katika familia na ndoa zao
zimeharibika na kusambaratika kabisa kutokana na kupata ushauri mbaya kutoka
walikopendelea kukaa mara nyingi.
Wengi wamejikuta wakifilisika na kuishi maisha ya umasikini chanzo kikiwa
ni mahali walipopendelea kukaa wakati wakiwa na mali.
Hata magonjwa mabaya na ya kutisha yamewapata wengi chanzo ni mahali
walipopendelea kukaa.
Ukisoma Biblia takatifu Marko 5:1-5, utaona habari za mtu aliyekaa
makaburini, makaburini ni sehemu inakowekwa miili ya watu waliofariki, si eneo
la kukaa watu lakini mtu huyu alikaa makaburini, neno linasema;-Na siku zote,
usiku na mchana alikuwako makaburini na milimani akipiga kelele na kujikata
kata kwa mawe.
Marko5:4 inasema;-mtu huyu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na
minyororo, akaikata ile minyororo na kuzivunja vunja zile pingu wala hakuna mtu
aliyekuwa na nguvu ya kumshinda.
Usishangae kumwona kijana anashauriwa na wazazi wake lakini hasikii lolote
na wala hajali,ndungu wamemshauri mwana familia wamekaa vikao visivyoweza
kuhesabika lakini hana wakumsikia, anaendelea kufanya jinsi apendavyo mwenyewe,
ni kwambie kwamba, mahali anapopendelea kukaa pamemfanya awe jinsi alivyo.
Mahali unapokaa panaweza kukufanya ufanye vitu vibaya vinavyo yaghalimu
maisha yako ni vyema na muhimu sana kutathimini kwa kina faida unayoipata
kutokana na sehemu au mahali unapopendelea kukaa mara kwa mara.
Na ukweli ni kwamba watu wengi wako
jinsi walivyo kutokana na mahali wanapopendelea kukaa na hata wewe huenda uko
hivyo ulivyo kutokana na hapo unapopapendele kukaa hivyo fanya uchunguzi
kubaini kama unavuna mabaya au mema kutoka sehemu au mahali unapopendelea kukaa
muda mwingi.
jamesmtiba@ gmail .com
No comments