Heade

KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI KENYA RAILA ODINGA KUAPISHWA

Mamia kadhaa ya waungaji mkono wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga wamekusanyika leo katika bustani katikati ya mji wa Nairobi, wakiwa na nia ya kumuapisha kuwa rais, kiongozi wao ambaye alisusia uchaguzi wa marudio mwaka jana.

 Rais Uhuru Kenyatta aliapishwa kutawala kwa muhula wa pili mwezi Novemba baada ya kushinda uchaguzi wa marudio mwezi Oktoba ambao Raila Odinga aliususia kutokana na shaka kwamba hautakuwa huru na wa haki. 

Licha ya kwamba polisi ilisema itapiga marufuku mkusanyiko wowote kinyume na sheria leo, hakuna polisi katika bustani hiyo na hakuna polisi wa kuzuia ghasia ama magari.

Aidha  Redio ya Capital FM mjini Nairobi imeripoti kuwa waungaji mkono wamepewa ruhusa na maafisa wa Kenya kuutumia uwanja huo.

No comments

Powered by Blogger.