Heade

MATAIFA YA AFRIKA YAMTAKA TRUMP KUOMBA MSAMAHA

Umoja wa Afrika unasema matamshi ya yanayodaiwa kutolewa na rais wa Marekani Donald Trump kuhusu bara Afrika ni wazi kwamba ni ya ubaguzi wa rangi.
Msemaji wa umoja huo , Ebba Kalondo, amesema toni la matamshi hayo lilikera hata zaidi ikikadiriwa idadi ya Waafrika waliouzwa kama watumwa Marekani.
Umoja huo unataka rais Trump aombe msamaha.
Inadaiwa kwamba rais Trump alitoa matamshi hayo dhidi ya Africa, Haiti na Elsavador kwenye ikulu ya White house katika mkutano na wabunge wa congress.
Baadaye rais Trump alikana kutoa matamshi hayo.
Matamshi hayo yamekashifiwa na wengi, likiwemo shirika la kimataifa kuhusu haki za binadam.
Image capti
Siku ya IJumaa bwana Trump alituma ijumbe wa Twitter akisema kwamba lugha aliyotumia wakati wa mkutano wake na wabunge wa Congress ili kuzungumzia swala la uhamiaji ilikuwa ngumu.
Lakini aliongezea kwamba maneno anayoshutumiwa kutoa sio lugha aliyotumia.
''Matamshi yalitolewa na Trump hayana heshima ya tofauti iliopo na haki za kibinaadamu''.
Uliongezea: Huku tukionyesha kushangazwa kwetu , Umoja wa Afrika unaamini pakubwa kwamba utawala mpya wa Marekani haulielewi bara la Afrika na watu wake.
''Kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo kwa mazungumzo kati ya utawala wa Marekani na mataifa ya Afrika''.

No comments

Powered by Blogger.