Heade

TANZANIA YAPATA NEEMA YA KUFANYA VIZURI KIUCHUMI



Tanzania imetabiriwa kufanya vizuri zaidi kiuchumi na wataalam wa masuala ya uchumi nchini baada ya kuibuka kinara wa Uchumi Jumuishi barani Afrika.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi, Bi. Bengi Issa amesema kuwa mabadiliko ya sheria katika sekta ya madini na katika umiliki wa makampuni ya simu yametoa fursa kwa watanzania wengi kushiriki katika uchumi.

Bi. Bengi Issa ameielezea dhana ya uchumi jumuishi kuwa ni ile ambayo shughuli za kiuchumi zinawajumuisha moja kwa moja wananchi hivyo kupitia mambo mbalimbali yanayofanywa na serikali kwa kuwashirikisha wananchi yatachochezea zaidi ukuaji wa uchumi.

“Serikali imeweka mazingira bora ya wananchi kushiriki shughuli za kiuchumi katika miradi mbalimbali, tunahakikisha kila mradi unaoingia nchini basi wafanyabiashara wa Tanzania wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo”, ameeleza.

Aidha Bi. Bengi amemaliza kwa kusema kuwa Uchumi jumuishi ndio msingi mkubwa wa kuleta amani na utulivu katika nchi kwani watu wanaguswa na matunda ya ukuaji wa uchumi ikiwemo serikali kufanikisha suala la kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi mpaka Sekondari.

No comments

Powered by Blogger.