Heade

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI AAGIZA VIWANDA 4 VYA SAMAKI VIFNGULIWE

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza viwanda vinne vya kuchakata minofu ya samaki vilivyofungwa vya Tan Perch Limited, Supreme Perch Limited, Mara Fish Packers Limited na Prime Catch Limited kufunguliwa ifi kapo Julai Mosi mwaka huu.
Pia Waziri Mpina ameagiza wamiliki wa viwanda hivyo vilivyofungwa vilivyoko katika mikoa ya Mwanza na Mara kuwasilisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi mpango kazi wa namna ya kuvifufua kabla ya kufikia mwezi Machi huu.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na maelfu ya Wavuvi katika Mwalo wa Bwai Kumsoma, Rorya na Mwalo wa Kisorya, Bunda, Mara, Waziri alisema hadi kufikia Juni mwaka huu samaki watakuwa wa kutosha Ziwa Victoria.
Pia Waziri Mpina alishiriki zoezi la kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye thamani ya Sh bilioni 3.2 zilizokamatwa na kikosi cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi Kanda ya Mara.
Alisisitiza msimamo wa Serikali ya awamu ya tano wa kuendelea kupambana na uvuvi haramu hadi pale utakapokoma katika Ziwa Victoria. Alisema operesheni hiyo maalumu ya kupambana na uvuvi haramu inayoendelea katika Ziwa Victoria haitakuwa na mwisho hadi pale uvuvi haramu utakapokoma na hakuna mvuvi haramu hata mmoja atakayesalimika katika ziwa hivyo kutakuwepo na ongezeko kubwa la malighafi ya samaki kwa ajili ya kuendesha viwanda hivyo.
Pia Waziri Mpina alimwagiza Katibu Mkuu wa Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Yohana Budeba kuandaa bei elekezi ya kununua samaki itakayowezesha kuondokana na tabia ya wenye viwanda kushusha ovyo bei samaki wanapoongezeka na kuwadhulumu wavuvi kupata malipo stahili yanayotokana na kazi yao Waziri huyo aliagiza maofisa Uvuvi wa Kijiji cha Bwai Kumsoma waliotuhumiwa kushirikiana na wavuvi haramu kuondolewa mara moja katika kijiji hicho ili kupisha uchunguzi na ikithibitika wachukuliwe hatua.
Kiongozi wa Kikosi cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi Kanda ya Mara, Bakari Lulela alisema operesheni hiyo imefanyika katika Wilaya za Musoma, Butiama, Rorya na Bunda.
Alisema wamefanikiwa kukamata na kuteketeza zana haramu zenye thamani ya Sh bilioni 3.2 huku wavuvi na wafanyabiashara wa samaki na mazao yake waliokiuka sheria ya uvuvi wakitozwa faini ya Sh milioni 189.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk Vincent Naano Anney alisema katika kuunga mkono mapambano ya vita dhidi ya uvuvi haramu iliyotangazwa na Waziri Mpina wamefanikiwa kukamata na kuteketeza zana haramu zenye thamani ya Sh bilioni 1.2 na Serikali ya wilaya hiyo itaendeleza kupambana na haramu bila kugopa vitisho wala mbinu chafu zinazofanywa na watu kwa lengo la kuwakatisha tamaa.

No comments

Powered by Blogger.