Heade

NI NANI ANAYEKUFUATILIA NYUMA MWAKA 2018 ?

Ni matuamaini yangu makubwa  kuwa unatamani kuona ukiendelea vizuri katika mipango yako na mambo mbalimbali uliyoyapanga na unayoendelea kuyapanga katika mwaka huu wa 2018.
Ni kukumbushe kuwa katika mipango mizuri ya kuyafikia malengo yako na kufika kule unakotamani kufika hakosi kuwepo adui anayekufuatilia nyuma ili kuyakwamisha malengo yako.
Watu wengi wamejikuta wakiwa watu wakupanga tu ,wanapanga mipango mingi na mambo makubwa lakini mipango hiyo yote huishia katika maandishi na meza za mazungumzo katika vikao walivyokaa.
Unaweza kujiuliza ni kwanini wakati wa kuanza mwaka ulipanga  mambo mazuri  na makubwa lakini mpaka sasa unaona tena kama hali iliyokutokea mwaka 2017 na miaka mingine iliyopita ya kutokufanikiwa katika mipango na malengo yako inataka kujirudia, unaweza kuwa unajiuliza maswali mengi lakini haupati majibu.
Ukisoma biblia takatifu katika kitabu cha Kutoka14:9-10 inasema Wamisri wakafuata nyuma yao,farasi zote na magari yote ya Farao na askari zake wenye kupanda farasi na jeshi lake, nao wakawapata hali wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni. Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao,na tazama wamisri wanakuja nyuma yao;wakaogopa sana;wana wa Israeli wakamlilia BWANA.
Wana wa Israeli walishikiliwa mateka nchini Misri kwa kipindi cha miaka mingi, wakiteswa mengi huko na kutumikishwa lakini Mungu akawahurumia akamtuma mtumishi wake Musa kwenda kuwaokoa baaada ya mvutano mkubwa uliokuwepo kati ya Musa na Farao , Farao akakubali kuwaachia wana wa Israeli waondoke Misri lakini walipoianza safari Farao akageuza mawazo akachukua jeshi lake kuwafuata wana wa Israeli ili jeshi liwakamate na kuwarudisha utumwani tena.
Hivi ndivyo ilivyo  hata sasa katika maisha  tunayoishi leo ,ndio maana unaona wakati unataka  kutoka kwenye utumwa wa madeni na hali mbaya ya kiuchumi yupo adui anayekufuatilia nyuma lengo lake akuzuie kupata fedha ili siku zote uwe mtu wa kudaiwa maana makusudi ya adui ni kukuona wewe unateseka.
Ndio maana unapanga mipango mizuri na wakati unapanga unaona uwezekano wa kufanikiwa ni mkubwa lakini unapojaribu kutekeleza uliyoyapanga unapata ugumu na vizuizi mbalimbali vya kukuzuia na hatimaye unakata tama.
Wana wa Israeli walipotazama nyuma wakaliona jeshi la Farao linakuja wakaogopa wakamlilia Mungu kwa sababu waliona Wamisri wamekaribia na wanataka kuwazuia lakini neno lisema wakamlilia Mungu.
Na Mungu aliye mwingi wa rehema akawahurumia kwa kuyatawanya maji na kufanya njia katikati mwa bahari nao wakapita na kuvuka ng'ambo suala ambalo lisingewezekana kwa mwanadamu awaye yote.
Hivyo nikwambie kwamba husikubali kushindwa na usiogope vikwazo,vizuizi na ugumu wowote unaouona katika mipango yako mwamini Mungu yeye anafanya njia pasipo kuwa na njia na atawafutilia mbali maadui wote wanaokufuatilia kama alivyo lifutilia mbali jeshi la Farao lililokuwa linawafuata nyuma wana wa Israel.
Mungu akulinde na kukupa ushindi kwa kila jambo jema ulifanyalo huu uwe mwaka wako wa kufanikiwa,AMEN.

No comments

Powered by Blogger.