Heade

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE MWAKA MMOJA KWA TUHUMA ZA KUEZUA NYUMBA MBILI AKIDAI KUWA MKE WAKE ANAMZALIA WATOTO WA KIKE PEKEE

Mwanaume mmoja aliye julikana kwa jina la Isaya Petro amehukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja kwa kosa la kuezua nyumba mbili huku akidai kuwa mke wake anamzalia watoto wa kike pekee.

Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mwanzo mugumu wilayani Serengeti mkoani mara Paskael Magau ametoa hukumu hiyo  jana baada ya mtuhumiwa kukiri kufanya kosa hilo.

Akitoa hukumu hiyo hakimu Magau amesema kuwa kwa kukiri kosa la kuharibu mali anamuhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja na kumtaka kurekebisha nyumba zote mbili alizoezua mabati ili familia ipate mahali pa kuishi.

Ameongeza kuwa wakati mtuhumiwa akiendelea kutumikia kifungo hicho hatakiwi kupatikana na kosa lolote katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa upande wake mke wa mtuhumiwa huyo Mariam Jackson mwenye umri wa miaka 33 amesema kuwa hukumu hiyo haikubainisha muda wa utekelezaji wake ambapo mpaka sasa anaishi kwenye chumba kimoja cha kupanga na watoto wake kwa msaada wa majirani.

No comments

Powered by Blogger.