Heade

MKUU WA WILAYA YA TARIME MH; GLORIOUS LUHOGA AWAAGIZA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA TARIME KUKUSANYA KODI KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

Mkuu wa wilaya ya Tarime mhe. Glorius Luhoga amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri ya Tarime vijijni na halmashauri ya mji wa Tarime kuanza kukusanya kodi kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu yanayochimbwa wilayani hapa ikiwa ni njia ya kuongeza pato la makusanyo ya ndani ya halmashauri hizo.

Agizo hilo amelitoa jana wakati akiongea na wenyeviti wa  vijiji na kamati za ulinzi na usalama vya kata ya Nyarokoba yaliyopo machimbo ya wachimbaji wadogo ya Mosege.

Mhe. Luhoga amesema kuwa wachimbaji hao wanapata pesa nyingi lakini hakuna utaratibu wowote uliowahi kuwekwa na halmashauri kuhakikisha kuwa wanalipa kodi kwaajili ya maendeleo yao na kuwa kitendo hicho kinarudisha nyuma nguvu ya serikali kufikisha maendeleo kwa wananchi.

Aidha ameziagiza kamati za ulinzi na usalama kuhakikisha migogoro ya ardhi iliyopo inatatuliwa ili kuwapa wananchi fursa ya kufanya maendeleo katika maeneo yao.

Naye kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime vijijni Bw. Peter Nyanja amesema kuwa jamii ya wakurya kwa sasa imepoteza msimamo uliokuwepo miaka ya nyuma kutokana na kutekeleza makubaliano yaliyokuwa yakiwekwa kila mara na jambo hilo linasababisha migogoro ya ardhi kuchukua muda kutatuliwa.


No comments

Powered by Blogger.