Heade

POLISI WAFANYA DORIA ..HALI IPO SHWARI HAKUNA MAANDAMANO

Makundi ya askari wakiwa wamebeba silaha, yameonekana leo asubuhi katika maeneo mbalimbali mjini Moshi.

Katika maeneo mbalimbali ikiwamo Soko la Mbuyuni, Manyema pamoja na soko la kati  watu wameonekana wakiendelea na shughuli zao.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah amesema hali iko shwari.

 Awali, kulikuwapo na tishio la maandamano leo katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

No comments

Powered by Blogger.