RAIS MAGUFULI; TUTAWASHUGHULIKIA WOTE WATAKAOUCHEZEA MUUNGANO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa mtu yeyote ataye jaribu kuuchezea muungano atashughulikiwa vikali hata kama atakuwa nje ya nchi.
Ameyasema hayo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo amesema kuwa kuna watu ambao hawapendi muungano uwepo lakini watu hao ni wa kupuuzwa.
Amesema kuwa muungano ni kitu kikubwa cha kujivunia hivyo Watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi zote zinazofanywa na Serikali.
“Muungano wetu ni mfano wa kuigwa duniani, kwasababu ni muungano wa kihistoria ambao ndio muungano ambao ni mfano katika mataifa mengine, lakini kuna watu ambao hata kama mkifanya vitu vizuri wenywe kazi yao ni kubeza tu, sasa nasema kwa yeyote atayejaribu kuuchezea muungano huu atachuliwa hatua kali haijarishi yuko ndani ya nchi ama nje ya nchi,”amesema Rais Dkt. Magufuli
No comments