ONGEZEKO LA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA LINAHITAJI SULUHU
Waziri wa elimu sayansi na Teknolojia Pr Joyce Ndalichako amesema kutokana na ongezeko la ukosefu wa ajira hususan kwa vijana nchini kuna umuhimu wa kutengeneza mazingira kwa ukuwaji wa biashara ili ajira nyingi zipatikane kiurahisi kwa vijana wanaomaliza elimu ya juu ili waweze kujiajiri.
Pr Ndalichako amesema tatizo la ukosefu wa ajira linaongezeka kutokana na kutokuwepo kwa uwiano wa ugavi na mahitaji kwenye soko la ajira pamoja na ongezeko la ajira kubakia katika sekta isiyo ya kilimo.
Aidha ameshukuru benki ya Barclays kwa kuwa mstari wa mbele kuisaidia serikali na jamii katika kuhakikisha tatizo la ukosefu wa ajira linatatuliwa na kupungua kwa kiwango kikubwa kwa kuwawezesha vijana.
No comments