Heade

MAKAMU WA RAIS ATARAJIWA KUFUNGUA KAMBI YA UCHUNGUZI MKURANGA

Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzani mhe. SAMIA SULUHU HASSAN anatarajiwa kufungua kambi ya uchunguzi wa macho, kisukari na shinikizo la damu katika  Wilaya ya Mkuranga mkoani PWANI.
Kambi hiyo itakayodumu kwa siku tatu imeandaliwa na klabu ya Lions ya Dar es salaam kwa kushirikiana na Hospitali ya Regency ya jijini humo ambapo kambi hiyo itatoa huduma bure kwa wananchi wote watakaojitokeza.

Mwenyekiti wa hospitali ya Regency Dk Rajni Kanabar amesema ufunguzi utafanyika siku ya jumamosi ambapo makamu wa rais Mhe,Samia Suluhu anatarajiwa kuwa  mgeni rasmi huku akisema kuwa wameamua kuandaa kambi hiyo ya bure baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wanasumbuliwa na maradhi hayo lakini wanakosa uwezo wa kwenda kupima.

No comments

Powered by Blogger.