Heade

SUMATRA YATAKIWA KUJA NA MBINU MPYA

Naibu waziri wa ujenzi, wa mawasiliano na uchukuzi Atashasta Nditiye ameitaka mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu {SUMATRA} kuwa na mbinu mpya zitakazosaidia kumaliza tatizo la ajali.
Nditiye akizungumza wakati alipotembelea  ofisi za sumatra na kukutana na watendaji wakuu wasumatra  amesema anaridhishwa na utendaji kazi wa mamlaka hiyo ila ni muhimu kwao kuja na mbinu na mawazo ya kibunifu kukabiliana na ajali zinazogharimu maisha ya watu wengi.

Aidha amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu na kujiweka mbali na vitendo vya rushwa huku wakizingatia kuendelea kuzingatia mapato yote yanafika mahali husika kwaajili ya maendeleo ya wananchi

No comments

Powered by Blogger.