WANAUME 12 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA
Polisi nchini inawashikilia wanaume 12 wakiwemo raia wa Afrika kusini n mmoja wa Uganda kwa tuhuma za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja katika oparesheni inayoendelea dhidi ya ushoga.
Kamanda wa polisi wa kanda maalum jijini Dar es salaam Lazaro Mambo sasa amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwenye hotel ya Peacok wakiwa wanahamasisha mapenzi ya jinsia moja ambapo kamanda huyo amesema sheria za Tanzania zinakataza uhusiano wa kimapenzi wa watu wa jinsia moja kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za Tanzania.
Mwezi mmoja uliopita watu 20 walikamatwa visiwani zanzibar katika oparesheni kama hii inayoendeshwa hivi sasa Tanzania bara.
No comments