RAILA ODINGA AMEKUTANA NA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI (IEBC) NCHINI KENYA
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini kenya Wafula Chebukati amekutana na mgombea urais wa upinzani Raila Odinga na kusema anatarajia kukutana na mgombea wa chama Tawala cha Jubilee Uhuru Kenyata.
Mwenyekiti huyo ameitisha mkutano wa wagombea urais wote leo mchana lakini akauhairisha mapema.
Hatahivyo rais Kenyata amesisitiza yuko tayari kwa uchaguzi huo na utaendelea pamoja na kuwa mgombea wa upinzani Raila Odinga alijiondoa wiki iliyopita.
Upande wa upinzani umekuwa ukishinikiza kuondolewa kwa afsa mkuu mtendaji wa tume hiyo Ezra Chiloba na maafsa wengine hatua ambayo haijatekelezwa na ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kinara wa upinzani Raila Odinga asusie kushiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu.
Hata hivyo hali hiyo imezidi kuumiza vichwa kwa pande zote mbili na kuyafanya Mataifa mengi ndani na nje ya Afrika kuitupia nchi hiyo macho kila uchao huku Uhuru Kenyata akiwaomba viongozi wa dini nchini humo kuwaongoza waumini wao kuliombea Taifa hilo.
No comments