WAOMBOLEZAJI THAILAND WATOA MACHOZI
Waombolezaji Thailand wanafanya matembezi kuadhimisha sehemu kuu ya siku tano za sherehe za mazishi kwa ajili ya mfalme Bhumibol Adulyadej aliyefariki oktoba 2016 akiwa na umri wa miaka 88.
Wajumbe wa familia ya mfalme wa Thailand na waheshimiwa kutoka nchi 40 watahudhuria mazishi hayo ya kuchomwa kwa mwili wa hayati mfalme Bhumimbol Adulyadej huku umati mkubwa wa watu ukitarajiwa kujipanga kwenye mitaa ya karibu.
Leo imetangazwa kuwa siku ya mapumnziko ambapo biashara nyingi zinafungwa kwa nusu siku au siku nzima kupisha maombolezo hayo badae siku ya ijumaa majivu ya mfalme yatasafirishwa hadi kwenye kasiri ya ufalme huku sherehe zikiendelea kwa siku mbili zaidi.
No comments