WATU 124 WAFARIKI KWA UGONJWA WA TAUNI NCHINI MADAGASCAR
Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na maradhi ya tauni nchini madagaska imefikia watu 124 huku serikali ikifaulu kupunguza ukali wa maradhi hayo kuendelea kutapakaa.
Waziri wa afya nchini humo amesema watu 1133 wameambukizwa maradhi hayo ikiwa miongoni mwao watu 780 wamepona huku wengine 290 wakiendelea kupatiwa matibabu.
Mkurugenzi wa WHO nchini madagaska Charlotte amesema wanashirikiana na serikali ya nchi hiyo katika kutoa msaada kwa waathirika wa maradhi hayo.
No comments