Heade

NG'OMBE WAPIGWE CHAPA KUKABILIANA NA WIZI WA MIFUGO

Naibu waziri wa mifugo na uvuvi mh Abdallah Ulega amewataka Viongozi wa halmashauri ya wilaya ya tarime mkoani mara  kuhamasisha na kusimamia zoezi la upigaji chapa kwa ng'ombe waliopo ili kukomesha wizi wa mifugo.
Naibu waziri  ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi hapa  wa halmashauri ya wilaya ya tarime huku akiwakumbusha wananchi kuwa ni jukumu la kila raia kulinda rasilimali za nchi kwa kuacha kuvusha mifugo kwenda nchi jirani suala ambalo litasaidia kukuza viwanda na uchumi wa mtanzania kwa kutumia rasilimali zilizopo kujiendeleza.
Aidha mh Ulega ameipongeza halmashauri kwa hatua ilizofikia ikiwemo kukomesha ukatili wa kijinsia,wizi wa mifugo mapigano ya koo na koo na kudhibiti uingizaji wa mifugo kutoka nchi za nje na kuahaidi kufungua mnada, na kuuboresha mnada wa kirumi ili kuweza kuruhusu wafugaji kunufaika na mifugo yao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya tarime mh Glorius Luhoga ameongeza kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana katika halmashauri  bado inakumbwa na changamoto mablimbali ikiwemo uhaba wa watumishi 127 katika kata na vijiji, vibali vinavyotumika kusafirisha mifugo tarime-sirari kusababisha kuvusha ng'ombe nchi jirani ya kenya na kupunguza umahiri wa minada iliyopo wilayani tarime.

Hata hivyo mkuu wa wilaya amesema ni vyema nchi jirani wakanunua mazao ya mifugo kuliko kununua mifugo na kurudisha mazao yake yakiwa na bei kubwa suala ambalo huchangia kuzorotesha viwanda nchini.

No comments

Powered by Blogger.