Heade

NAIBU WAZILI WA MIFUGO NA UVUVI AWATAKA MAAFISA FOROZA KUONGEZA JUHUDI

Naibu waziri wa mifugo na uvuvi mhe.Abdallah Ulenga amewataka maofisa wa forodha sirari Wilayani Tarime kuongeza juhudi katika kulinda rasirimali ili kuunga mkono juhudi za rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.JOHN POMBE MAGUFULI za kulinda rasirimali za nchi.
Ameyasema hayo baada ya kufanya ziara Wilayani Tarime na kuelezwa kuwa wilaya ya Tarime haina tatizo la mifugo kutoka nje ya nchi na kuingia nchini isipokuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya madalali kutorosha mifugo na kuiuza nchi jirani ya Kenya.
Hivyo amewataka watendaji hao kusimamia sheria na kufanya kazi kwa uadilifu ikiwemo kushirikiana ili kudhibiti hali hiyo inayorudisha nyuma jitihada za serikali za kuleta maendeleo.

Aidha Ulenga ametumia nafasi hiyo kuwaeleza watumishi hao kwamba wizara itahakikisha kituo cha ukaguzi wa mifugo cha kirumi kinafanya kazi kwa ufanisi kwa kuweka miundombinu ya maji na umeme ili mnada uliopo uanze kufanya kazi.

No comments

Powered by Blogger.