Heade

ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS ZIMBABWE ATOLOKA NCHINI HUMO

Aliyekuwa makamu wa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aliyefutwa kazi siku ya jumatatu ametoroka Taifa hilo kufuatia vitisho vya kifo kulingana na washirika wake.
Rais Mugabe amemshutumu Mnangagwa kwa kupanga njama za kuchukua mamlaka kutoka kwake akidai kuwa makamu huyo alienda kanisa moja ili kujua mgabe atafariki lini ambapo alipokea taarifa za kufariki yeye kabla ya Mugabe.

Katika suala hilo Mugabe amemtaja Naibu wake wa zamani kuwa miongoni mwa waliopanga njama na kuonya kuwa atawachukulia hatua maafisa wengine wa chama hicho walioshirikiana na Mnangagwa.

No comments

Powered by Blogger.