RAILA ODINGA APENDEKEZA KUUNDWA SERIKALI YA MUDA NCHINI KENYA
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amependekeza kuundwa kwa serikali ya muda nchini humo na kutawala kwa muda wa miezi sita kama sehemu ya kutatua mzozo wa kisiasa unaoendelea
Amesema katika kipindi hicho kunafaa kufanyika marekebisho ya katiba kwa kuchunguza upya mamlaka ya rais huku akisema kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta kuhusu marekebisho ya kikatiba ambayo yanahitajika ili kupunguza hatari ya kuzuka kwa fujo kutoka kwa makundi ya jamii za wachache wanaojiona kuwa wametengwa
Mhe Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu ambapo alipata kura milioni 7.5 ambazo ni sawa na asilimia 98 ya kura zilizopigwa.
No comments