Heade

ANAEOLOWA AWE NA LIVING CERTIFICATE

Naibu Waziri Ofisi ya Rais tamisemi Mh. Joseph Kakunda amewatahadharisha viongozi wa dini  nchini kujihadhari  kuwaozesha wasichana ambao hawajamaliza elimu ya kidato cha nne ili kuepuka kukumbwa na mkono wa sheria

Mhe. Kakunda ameyasema hayo alipokuwa wilaya ya Nkasi  na kuongeza kuwa watoto wa kike wanashindwa kumaliza masomo kwasababu ya mimba ama kuozeshwa jambo ambalo limeendelea kuisumbua serikali katika juhudi zake za kuokoa maisha ya watoto wa kike ili waendelee na masomo 
Amefafanua kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inathamini sana maisha ya watoto wa kike na inaendelea kuweka mikakati ya kila namna ili kuhakikisha kuwa wasichana hao wanapata elimu stahiki, kwa kuanza na elimu bure 

Amesema kuwa tunakoelekea ili binti aolewe lazima awe na Leaving Certificate na kuongeza kuwa mwananfunzi ambae ataolewa kwa kukatishwa masomo wazazi wake wakamatwe na vilevile na wazazi wa pande mbili wa aliyeoa, aliyeolewa, wanaoshangilia,na aliyefungisha ndoa wote wafunguliwe mashitaka.

No comments

Powered by Blogger.