CDF WATOA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE WILAYANI TARIME
Shirika lisilo la kiserikali la CDF linalotetea haki za watoto limetoa elimu juu ya kupinga ndoa za utotoni,ukeketaji pamoja na mimba za utotoni kwa wasichana kutoka kata tano wilayani Tarime
Bi Donathea Erenest ni afisa ufatiliaji na tathimini katika shilika hilo amesema kuwa semina hiyo inalenga kukuza haki za watoto hasa wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia elimu ya jinsia na afya ya uzazi
Bi Donathea ameongeza kuwa kumekuwa na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike kama ukeketaji,kulazimishwa kuolewa,kutopewa fursa ya elimu kutosikilizwa na vipigo jambo ambalo ni ukiukwaji wa haki za binadamu
Kwa upande wao wasichana na wahanga wa matukio mbalimbali walioshiriki kutoka katika kata za Pemba,Regicheri,Mbogi,Komaswa,na Binangi wamelishukuru shilika hilo la CDF kwa semina hiyo iliyo wapatia mwanga wa kuzijua haki zao za kimsingi na kuomba semina hizo ziwe endelevu
No comments