Heade

HALMASHAURI YA KISARAWE MKOANI PWANI IMETOA MIKOPO KWA VIKUNDI



Halmashauri ya kisarawe mkoani Pwani imetoa kiasi cha shilingi milioni 102 kuvikopesha vikundi vya wajasiriamali vipatavyo 49, vikundi vya akina mama, vijana na walemavu kuwawezesha kuendesha shughulkuli mbalimbali za biashara.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi hundi ya fedha hizo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Bw Musa Gama amesema fedha hizo za mikopo zimepatikana kwa  makusanyo ya mapatao ya ndani na zimetolewa kwa vikundi hivyo katika kata zote 17 ikiwa ni hatua ya kuunga juhudi za rais John Pombe Magufuli kukuza uchumi wa viwanda.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Happynes Seneda ameviasa vikundi vyote vilivyopata mkopo kuzitumia fedha hizo vizuri kwa shughuli zitakazoleta manufaa kwa jamii na kwa Taifa kwa ujumla.

No comments

Powered by Blogger.