DOLNARD TRUMP AFANYA UTEUZI.
Rais wa Marekani Donald Trump amemteuwa Jerome Powell kuwa mwenyekiti mpya wa benki kuu ya Marekani.
Powell mwenye umri wa miaka 64 aliyekuwa zamani mwekezaji vitega uchumi anachukua nafasi ya Janet Yellen anayemaliza muda wake mwezi Februari mwaka ujao. Trump amemsifu bwana Powell kuwa mtu madhubuti na mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi.
Bwana Powell ameahidi kuwa atakapoanza kuutumikia wadhfa huo atafanya kila litakalo wezekana kudumisha uthabiti wa bei na kufikia kiwango cha juu cha ajira huku Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaamini kwamba mwenyekiti huyo mpya ataendeleza sera ya bi Yellen ya wastani katika riba.
No comments