MH: RAIS MAGUFULI AMWANDIKIA WAZIRI MKUU WA CANADA BARUA
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. JOHN pombe Magufu amemwandikia
barua waziri mkuu wa Canada akimtaka
ashughulikie kwa haraka suala la ndege ya Bombandier Q 400 inayo shikiliwa nchini humo.
ndege hiyo ni miongoni mwa ambazo mh rais aliahidi kununua ikiwa ni
mikakati ya kulifufua shirika la ndege la Tanzania ATCL .
Mh. rais akizungumza katika uzinduzi
wa uwanja wa ndege mjini bukoba amesema
licha ya kuandika barua kwa waziri mkuu wa canada amemtuma mwana sheria mkuu wa
serikali George Masaju kwenda nchini humo kushughurikia swala hilo
kisheria
Wakati
huohuo mhe. rais ameamuru kukamatwa kwa watumishi watatu wa serikali kwa tuhuma
za kuandika madai yasio halali yakiwa na lengo la kuiibia serikali
No comments