NGOME YA KUNDI LA ISLAMIC STATE (I S) YATEKWA NA MAJESHI YA SYRIA
Shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake nchini Uingereza limeripoti kwamba majeshi ya serikali ya Syria yameiteka ngome kuu ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS iliyopo mashariki mwa nchi hiyo.
Mji wa Deir al Zor wenye utajiri wa mafuta uliokuwa chini ya magaidi hao tangu mwaka 2014 sasa umo katika udhibiti kamili wa vikosi vya serikali ya Syria.
Magaidi wanaojiita Dola la Kiislamu mnamo wiki zilizopita walikuwa tayari wameshanyang'anywa maeneo zaidi huku wapiganaji wa IS wamerudishwa nyuma hadi kwenye eneo karibu na mto Euphrates na kwenye maeneo ya jangwani.
No comments