WANANCHI WA WILAYA YA TARIME WATAKIWA KUTUMIA MPAKA WA SIRARI VIZURI
Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe. Hamadi
Masauni amewataka wananchi na wafanya biashara wanao fanya shughuri zao karibu
na kituo cha mpaka wa sirari unao
tenganisha nchi ya Tanzania na kenya
kuhakikisha wanashirikiana na jeshi la polisi mkoani mara kudhibiti matukio ya
uhalifu.
Ameyasema hayo akiongea na wananchi wakati wa ziara yake
ya kikazi katika mkoa wa mara ikiwa na lengo la kutembelea mipaka iliyopo
mkoani mara inayo tenganisha Tanzania na nchi jirani za kenya na uganda ambapo
amesema kuwa mara nyingi kumekuwa na taarifa za wananchi wa mipakani
kushirikiana na uhalifu kupitisha mali za magendo suala ambalo ni hatari.
Hivyo amewataka wananchi hao kuwacha tabia hiyo inayokuwa
kwa kasi katika eneo la mpaka na kulisisitiza jeshi la polisi kufanya kazi yake
kikamilifu na kwa yeyote atakae baina kutumia mpaka kinyume na utaratibu
atakumbana na mkono wa sheria.
No comments