Heade

KAMPUNI YA MABASI YA KILIMANJARO EXPRESS YASITISHIWA HUDUMA YA USAFIRI

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imesitisha utoaji huduma za usafiri kwa kampuni ya mabasi ya kilimanjaro express ltd baada ya kushindwa kulipa kodi ya shilingi milioni mia tano.
Akizungumza na waandishi wa habari mkurgenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA Richard Kayombo amesema wamefika uamuzi huo baada ya majadiliano ya muda mrefu na uongozi wa kampuni hiyo kutokuzaa matunda.
Ameongeza kuwa kwa kipindi cha hivi karibuni biashara haikuwa nzuri kwa kuwa mabasi yake 26 yalipungua hadi 12 lakini hicho hakikuwa kigezo cha kutokulipa kodi serikalini.
Kwa upande wake mmliki wa kampuni hiyo Roland Sawaya amesema wamezuia mabasi yake ambayo yalikuwa yameegeshwa katika ghala mjini moshi mkoani kilimanjaro huku akieleza kuwa amekuwa akilipa deni hilo kwa awamu.
Hata hivyo amesema kuwa hivi karibuni alilipa shilingi milioni 50 na mwezi huu walitaka kulipa shiling milioni 35 lakini TRA walikataa na kuwataka kulipa kiwango chote huku akieleza kuwa mazungumzo yanayoendelea ana imani yatafikia muafaka.


No comments

Powered by Blogger.