MKUU WA MKOA WA MARA AMEKUTANA NA WATUMISHI
Mkuu wa mkoa wa mara mhe.Adam Malima amekutana na watumishi wakuu wote wa mkoa wa mara kwa lengo la kuweka mambo wazi yanayotakiwa kutekelezwa ikiwemo kuweka mikakati ya pamoja suala ambalo litapelekea kuwepo kwa maendeleo mkoani humo.
Hayo yamebainishwa katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa CMG tarime ambapo mkuu wa mkoa amesema kuwa kumekuwepo na viongozi wasio kuwa watendaji katika kazi zao jambo linalo kwamisha shughuli za maendeleo.
Aidha mkuu wa mkoa amesema lengo la kikao hicho ni kutoa na kupokea taarifa za sekta zote zilizopo katika mkoa wa mara kupitia viongozi wake wakuu huku akiipongeza kamati ya ulinzi na usalama kwani mpaka sasa mkoa wa mara unasifika kwa kuwa na ulinzi wa kutosha.
Hata hivyo nao baadhi ya wakuu wa idara waliohudhuria kikao hicho kutoka ofisi ya vitambulisho vya taifa NIDA mkoa wa mara Bi Ohana Gerald amesema kuwa changamoto wanayokumbana nayo ni pamoja na mwitikio mdogo kutoka kwa wananchi ambapo mpaka sasa katika mkoa wa mara watu waliojiandikisha ni elfu themanini na mbili na thelathini na sita tofauti na matarajio yao ambapo walitarajia kuandikisha watu milioni moja na laki mbili
No comments