Heade

WAZAZI WATAKIWA KUWALEA VIZURI MABINTI WA KAZI

Wakazi wa Tarime wameombwa kujenga utamaduni wa kuishi vizuri na mabinti wa kazi kwani mabinti hao wamezifikia familia zao ili ziwe sehemu ya faraja katika maisha yao.
Akifundisha wakati wa semina ya neno la Mungu katika kanisa la EAG(T), Buhemba kwa Mchungaji Thomas Ryoba  wilayani Tarime ,mtumishi wa Mungu, mchungaji na mwimbaji wa nyimbo za injili Abiud Mishori kutoka jijini mbeya amewataka wazazi wanaokaa na mabinti wa kazi wawafanye kuwa miongoni mwa watoto wao na wawalee kama wanavyowalea watoto wao na si kuwanyanyasa kwa kuwatumikisha kupita kiasi na kuwacheleweshea mishahara.
Amesema Mungu huwaleta mabinti hao ili wawe sehemu ya watoto wa familia na si kuwafanya watumwa jambo ambalo halimpendezi Mungu.
Mch. Abiud amesema kuwa mabinti wa kazi wakilelewa vizuri nao pia huwalea vema watoto wanao achiwa wakati wazazi wanapokuwa mbali na familia zao,amesema mabinti hao wana nafasi kubwa katika makuzi na tabia za watoto kwani mara nyingi hukaa na watoto.
Pia alitumia nafasi hiyo kuwaombea mabinti wa kazi kutoka familia mbalimbali huku wengi wakifunguliwa kutoka katika vifungo vya shetani wakati wa maombezi hayo.

No comments

Powered by Blogger.