MAANDALIZI YA KUMUAPISHA RAIS UHURU KENYATA YAKAMILIKA
Ulinzi umeimarishwa katika jiji kuu
la Kenya, Nairobi pamoja na miji mingine mikuu huku Rais Uhuru Kenyatta
akitarajiwa kuapishwa kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine hapo kesho.
Kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga amepanga kuandaa mkutano mkubwa wa kuwakumbuka watu waliofariki wakati wa makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na polisi.
Bw Odinga na muungano wake wa National Super Alliance (Nasa) wamesisitiza kwamba mkutano huo utafanyika katika uwanja wa Jacarada, Nairobi, takriban kilomita kumi hivi kutoka uwanja wa Kasarani ambapo sherehe ya kuapishwa kwa Bw Kenyatta itakuwa ikiaendelea.
Hata hivyo polisi wamesisitiza kwamba hakutakuwa na mkutano mwingine Nairobi ila sherehe ya kumuapisha Rais Kenyatta.
Serikali imesema viongozi 20 wa mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Bw Kenyatta, akiwemo kiongozi wa chi jirani ya Tanzania Dkt John Magufuli.
No comments