Heade

MAHAKAMA YA MUHUKUMU YA MTOTO WA CHACHA WANGWE

Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imemhukumu mtoto wa aliyekuwa mwamasisasa nguli marehemu Chacha Wangwe , Bob Wangwe kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela au faini ya shilingi milioni 5 kwa makosa ya mtandao.
Mahakama imemhukumu Bob Wangwe baada ya kupatikana na hatia kwwenye kosa la kuchapisha taarifa za uongo na kupotosha kwenye mtandao wa facebook machi 15 mwaka jana.
Hakimu huyo amesema Bob amekutwa na hatia chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015 ambapo katika utetezi wake Bob aliomba apunguziwe adhabu kwa sababu ni mwanafunzi wa masomo ya sheria na bado ni kijana mdogo na hilo ni kosa lake la kwanza kulitenda  

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi mkuu Huruma Shaidi ambapo amesema katika kesi hiyo upanade wa mashahidi ulikuwa na mashahidi 6 na vielelezo vitano dhidi ya Bob ambaye pia ni mwanaharakati .

No comments

Powered by Blogger.