Heade

WANANCHI AUSTRALIA WAPIGA KURA KWA WINGI KUHALALISHA NDOA YA JINSIA MOJA

Wananchi wa Australia wamepiga kura kwa wingi kuhalalisha ndoa za jinsia moja .
Zaidi ya watu milioni 12.7 karibu asilimia 79.5 ambao ni wapiga kura walishiriki katika zoezi hilo kwa majuma manane ambalo liliongozwa na swali moja lililohoji kama sheria ya ndoa inaweza kubadilishwa kuruhusu wapenzi wa jinsi moja kufunga ndoa.

Kura hiyo ya kihistoria imeonyesha kuwa asilimia 61.6 ya watu wamepiga kura kuruhusu wapenzi wa jinsi moja kufunga ndoa huku wapiga kura hao wakizagaa maeneo mbalimbali ya umma wakisherehekea  kwa kuiimba na kucheza.

No comments

Powered by Blogger.