Marekani imeyataka
mataifa yote kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na
Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la
masafa marefu.
Akizungumza katika baraza la usalama la umoja wa
kimataifa ,mjumbe wa Marekani katika baraza hilo Nikki Haley amesema
kuwa rais Trump amemtaka mwenzake wa China kukata usambazaji wa mafuta
kwa Pyongyang.
Amesema kuwa Marekani haitaki mzozo lakini Korea Kaskazini itaangamizwa iwapo vita vitazuka.
Onyo hilo linajiri baada ya Pyonyang kufanyia majaribio kombora lake la kwanza katika kipindi cha miezi miwili.
Korea
Kaskazini imesema kuwa kombora hilo lililorushwa siku ya Jumatano
ambalo inasema liliruka kimo cha kilomita 4,475, ikiwa ni mara kumi
zaidi ya kimo cha kituo cha angani.
Madai hayo hayakuthibitishwa na wataalam wametiliashaka uwezo wa taifa hilo kuwa na teknolojia kama hiyo.
Hatahivyo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa uzinduzi wa kombora hilo ulikuwa wa kufana.
Jaribio
hilo likiwa mojawapo ya majaribio yaliofanywa na taifa hilo
limeshutumiwa na jamii ya kimataifa na tayari baraza la usalama la umoja
wa kimataifa limeitisha kikao cha dharura.
Bi Haley alionya kuwa kuendelea kwa uchokozi kunalenga kuliyumbisha eneo hilo.
''Tunahitaji China kuchukua hatua zaidi'', alisema.
Rais
Trump alimpigia simu rais Xi Jinping mapema siku ya Jumatano , Ikulu ya
Whitehouse ilisema kuwa rais Trump alizungumza na Xi Jinping kwa simu
akimtaka kuchukua hatua zozote kuishawishi Korea Kaskazini kusitisha
uchokozi na kusitisha mpango wake wa kinyuklia.
No comments