Muungano wa Upinzani wa Rassemblement nchini
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo umeitisha maandamano ya nchi nzima hivi
leo kumshinikiza rais Jospeh Kabila kuondoka madarakani kufikia mwisho
wa mwaka huu.
Upinzani pia unataka kuwepo kwa serikali ya mpito kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.
Mwenyekiti
wa muungano huo Felix Tshisekedi pia ametupilia mbali mswada wa sheria
za uchaguzi na kusema kuwa zinahatarisha mchakato mzima na wakati huo
huo kuwataka wananchi wajitokeze kwa uwingi kuhishiriki maandamano ya
hii leo.
Hata hivyo serikali ya DRC imepiga marufuku maandamano hayo ikisema kuwa ni kutokana na sababu za kiusalama.
Kumekuwa
na shinikizo kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa, kwa serikali ya DRC
kuhakikisha kuwa Uchaguzi huo unafanyika kama ilivyopangwa.
Polisi
jijini Kinshasa katika siku zilizopita, wamekuwa wakikabiliana na
waandamanaji wa upinzani kwa kuwakamata na hata kuwafwatulia risasi na
mabomu ya kutoa machozi.
Watu kadhaa walikamatwa na wengine
kujeruhiwa katika mandamano yaliyofanyika hivi karibuni katika miji ya
Goma na Bukavu, mashariki mwa DRC, kumshinikiza rais Kabila ajiuzulu
kabla ya tarehe 30 Desemba mwaka huu.
No comments